SIMAMIENI MIRADI YA MAENDELEO KWA WELEDI’ MHE. GIDARYA

SIMAMIENI MIRADI YA MAENDELEO KWA WELEDI’ MHE. GIDARYA

Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata mkoani Simiyu wameagizwa kusimamia kwa weledi utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kwenye maeneo yao ili fedha zinazopelekwa na Serikali zilete matokeo na kuwaondolea changamoto wananchi. Kauli hiyo ya Serikali imetolea leo tarehe 23.04.2924 mjini Bariadi mkoani Simiyu na Mheshimiwa Anna Gidarya Mkuu wa Wilaya ya Itilima ambaye alifunga mafunzo

Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata mkoani Simiyu wameagizwa kusimamia kwa weledi utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kwenye maeneo yao ili fedha zinazopelekwa na Serikali zilete matokeo na kuwaondolea changamoto wananchi.

Kauli hiyo ya Serikali imetolea leo tarehe 23.04.2924 mjini Bariadi mkoani Simiyu na Mheshimiwa Anna Gidarya Mkuu wa Wilaya ya Itilima ambaye alifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Dkt. Yahaya Nawanda.

“Serikali inapeleka fedha nyingi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, nasisitiza mkafuatilie na kusimamia vizuri fedha za miradi inayoletwa na Serikali katika maeneo yenu ili fedha hizo zilete matokeo tarajiwa na kuwaondolea wananchi changamoto za kukosa huduma” alisema Mhe. Anna Gidarya.

Aidha, amewataka kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwenye maeneo yao kama kipaumbele cha Serikali sambamba na kutumia mifumo ya kielektroniki wanapokusanya mapato ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali pamoja na kusaidia kubuni vyanzo vya mapato vitakavyosaidia Halmashauri zao kuongeza mapato ya ndani kila mwaka.

Katika hatua nyingine Mhe. Gidarya amewataka viongozi hao kuhakikisha usalama, amani na utulivu vinakuwepo kwenye maeneo yao kwa kushirikiana na vyombo vya usalama pamoja na kujenga mahusiano mazuri kwa wananchi ili kusaidia kutoa taarifa za uvunjifu wa amani bila kuwa visababishi vya wananchi kukosa imani nao kwa kuvuruga amani na usalama.

Kwa upande wake Ibrahim Minja Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais-TAMISEMI alisema lengo la mafunzo hayo ni kwajengea uwezo ili kuweza kusimamia miradi kwa ubora na thamani halisi ya fedha.

Naye Isack Lwela Mtendaji wa Kata Halmashauri ya Wilaya ya Maswa alisema ameiomba Ofisi ya Rais TAMISEMI kuziagiza Halmashauri nchini kujenga ofisi za Watendaji wa Kata, kuzipatia samani pamoja na fedha za uendeshaji wa ofisi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »